DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 12, 2024 amekagua ujenzi wa Mnara wa Mashujaa uliopo mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika Dodoma, Julai 25, 2024.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mnara huo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi na amemtaka mkandarasi wa mnara huo ambaye ni Suma JKT kukamilisha ujenzi kwa viwango na ubora ifikapo Julai 22, mwaka huu.
