LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC),Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, alipowasili wilayani Ruangwa kwa ajili ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa na maandalizi ya Jubilei ya miaka 25 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Wolfgang na miaka 50 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Bruno Ngonyani, ambaye ni Aksofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Lindi.