Waziri wa Fedha, Dkt.Nchemba awataka Watanzania kupuuza uongo uliozushwa na Tanzanialeaks kuhusu Hazina

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Fedha,Mheshimiwa Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania kupuuza taarifa iliyosambazwa na Tanzanialeaks ikidai Tanzania imefilisika.

Mheshimiwa Waziri Dkt.Nchemba ametoa wito huo leo Julai 19,2024 kupitia kurasa zake za kijamii akikanusha taarifa iliyozushwa na mtandao huo ikidai Hazina kumekauka.

"Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, ameandika hatujalipa Bwawa- Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

"Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa.

"Malipo yameendelea kulipwa kwenye sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo.

"Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya," amefafanua Waziri Dkt.Nchemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news