ZIPA yamshirikisha jambo Balozi Kasike

ZANZIBAR-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mhe. Phaustine Kasike amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Bw. Saleh Saad Muhammed.
Mkutano huo umefanyika kwenye Ofisi za ZIPA zilizopo Maruhubi, Zanzibar ambapo Bw. Muhammed aliuomba Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Msumbiji kuisaidia ofisi yake kutafuta wawekezaji kutoka Msumbiji kwa ajili ya kuja kuwekeza Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.

Aidha, Bw. Muhammed aliuomba Ubalozi kuunganisha ofisi yake na taasisi zinazohusika na Uwekezaji nchini Msumbiji ili kuanzisha ushirikiano kwa maslahi ya nchi zetu.
Pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi Kasike aliahidi kuiunganisha ZIPA na Taasisi za Uwekezaji za Msumbiji kama ilivyoombwa na ZIPA.Aidha, aliushauri Uongozi wa ZIPA kuwasiliana na Uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ili kujadiliana namna Zanzibar itakavyonufaika baada ya Kituo hicho kusaini Mkataba wa Ushirikiano na Wakala wa Ukuzaji Uwekezaji na Usafirishaji wa Bidhaa za Msumbiji Nje ya nchi (APIEX) wakati wa Ziara ya Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, iliyofanyika Tanzania hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news