Ajali basi la Baraka na lori yaua mkoani Pwani

PWANI-Abiria wanne akiwemo mtoto mdogo wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Baraka na Lori katika eneo la Vigwaza lililopo Chalinze mkoani Pwani.
Ajali hiyo imetokea Agosti 22, 2024 wakati basi hilo likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, likijaribu kuyapita magari mengine mbele yake na kukutana na lori na kugongana uso kwa uso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha ajali hiyo na kusema waliofariki ni watu wanne.

Lutumo ameongeza kuwa,majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Kituo cha Afya Mlandizi Kibaha ili kupata matibabu huku miili ya waliopoteza maisha ikihifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge alifika eneo la tukio na kuwataka madereva kuacha kukiuka sheria za usalama barabarani huku akitoa pole kwa wafiwa na kuwatakia uponaji wa haraka majeruhi wa ajali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news