Aliyekuwa Mwalimu wa chuo hatiani kwa rushwa ya ngono

DAR-Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imemhukumu aliyekuwa mwalimu wa Chuo cha Afya Paradigm,Bw.Shadrack James Mayala adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh. 200,000.
Ni baada ya kukutwa na hatia katika kosa la Rushwa ya Ngono kinyume na Kifungu cha 25 Cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Marejeo ya Mwaka 2019.

Kifungu ambacho kinasomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza pamoja na vifungu vya 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura 200 Marejeo ya mwaka 2019.

Hukumu dhidi ya Bw. Shadrack James Mayala imetolewa Julai 31, 2024 kutokana na shauri la Uhujumu Uchumi Na. 04/2023 lililokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Mkazi Nabwike Mbaba.

Shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni, Mbumi Kisiku.

Ilielezwa kuwa mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Aprili 29, 2023 kwa shtaka la kushawishi kupata ngono kutoka kwa mwanachuo (jina limehifadhiwa) ili aweze kumsaidia namna ya kufaulu mitihani iliyokuwa ikimkabili mwanafunzi huyo.

Mahakama katika hukumu yake imemkuta mshtakiwa na hatia na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya shilingi 200,000, ambapo mshtakiwa amelipa faini hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news