Asasi za Kiraia kupitia FCS zaiangukia Serikali digitali kwa makundi maalum nchini

DAR-Asasi za Kiraia nchini kupitia Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), zimeiomba Serikali iangazie katika kuhakikisha makundi maalum yanawezeshwa kufikia miundombinu ya kidigitali ili waweze kushiriki katika michakato ya maendeleo na kujiimarisha kiuchumi.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.

Hayo yamesemwa na Meneja Programu wa FCS Bi. Nasim Losai katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani na wadau, uliofanyika Agosti 12, 2024 jijini Dar es salaam.

Bi. Losai amesema kuwa mkutano huo umejikita katika kuangazia ushiriki wa watu wenye ulemavu katika maendeleo, uchumi na kijamii, huku ukiangazia matumizi ya takwimu za sensa katika kuboresha mipango ya halmashauri za wilaya na ngazi za kata.
Meneja Programu wa FCS Bi. Nasim Losai katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani na wadau, uliofanyika Agosti 12, 2024 jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali imekuwa Sikivu katika kuhakikisha makundi maalum yanafikiwa na kuwezeshwa katika shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato, nakwamba FCS wamekuwa wakIisadia serikali katika kuunga mkono juhudi hizo kutokana na zoefu wao wa zaidi ya miaka 20 ya kufanya kazi na jamii.

"FCS tuna zaidi ya miaka 20 tumekuwa tukisaidia serikali hasa katika shughuli za jamii na kutetea watu wenye ulemavu na michakato ya kiserikali, hasa kwenye majengo mengi mioundombinu imebadilika na kazi kubwa imefanywa na FCS pamoja na makundi haya," amsema Bi. Losai.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.

Kwa upande wake Mshauri wakitalam masuala ya watu wenye ulemavu Tanzania Peter charlse, amesema mkutano huo umejumuisha watu mwenye ulemavu zaidi ya 600 kutoka ndani ya Jiji la Dar es salaam wakiwepo madiwani 60 wa viti maalimu na wale wakuteuliwa.

Amesema kuwa malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali na kuangazia zaidi eneo la uchumi na kuona fursa zipi walemavu wameweza kushirikishwa na ambazo wanaziweza.
Mshauri wakitaalam masuala ya watu wenye ulemavu Tanzania, Peter Charles Mwita akizungumza kwenye mahojiano na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano huo jijini Dar es Salaam.

"Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu bado ni mdogo ndio maana tumewaalika madiwani ili kuangalia changamoto zilizopo na kuwajengea ili kuyaingiza katika mipango yao ya maendeleo kupitia Mabaraza yao ndani ya halmashauri,"amesema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania Hamadi Abdallah komboza, amesema changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni masuala ya ajira, huku akimuomba kamshina wa kazi na vyama vyenye ulemavu kufanya ukaguzi kwenye mashirika na taasisi ambazo zinapaswa kuajiri watu wenye ulemavu lakini bado hazijatekeleza nakwamba msukumo zaidi unahitajika.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.

Katibu Mkuu Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania, Jonas Lubalo ameishukuru taasis ya Ikupa Trust Fund kwa kuendelea kuchangia na kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news