KAGERA-Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa Vitambulisho vya Uraia (NIDA) kwa wananchi wa Ngara mkoani Kagera, wanaokidhi vigezo.


Akiwa ameambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa katika ziara hiyo; Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Ndugu Rabia Hamid Abdallah, Balozi Nchimbi ameielekeza Wizara hiyo kuchukua hatua haraka ili changamoto hiyo imalizwe.
Amesema hata utaratibu wa kuruhusu watu kuazimana vitambulisho vya NIDA kwa shughuli mbalimbali ni jambo hatari, linaloweza kusababisha uhalifu.
"CCM itasimamia ili kuhakikisha suala hilo linafanyiwa kazi na kasi ya utoaji wa vitambulisho vya NIDA inapatikana," amesema Dk. Nchimbi.