Benki ya Dunia yaipongeza Tanzania ujenzi Mradi wa SGR

NA BENNY MWAIPAJA
WF Abuja

BENKI ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyopiga katika kutekeleza mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa-SGR kwa kuwa ni miongoni mwa miradi itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kushoto), akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, wakati walipokutana kando ya Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria, ambao unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.

Pongezi hizo zimetolewa mjini Abuja nchini Nigeria na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, alipokutana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Kando ya Mikutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Nchi za Afrika, ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia na Shiruka la Fedha la Kimataifa-IMF.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, akizungumza wakati wa kikao chake na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), kando ya Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule.

Dkt. Victoria Kwakwa, amesema kuwa si rahisi kwa nchi nyingi za Afrika kujenga mradi mkubwa wa reli kama ilivyofanya Tanzania kwa kuwa ina gharama kubwa lakini kukamilika kwake kutachochea biashara katika eneo la Maziwa Makuu huku akimmwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzindua rasmi safari za treni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati), wakiwa katika Kikao na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa (hayupo pichani), kando ya Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule.

Kwa upande wao, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba, walipokea pongezi hizo kwa niaba ya Serikali na kueleza kuwa lengo la mradi huo ni kuunganisha baadhi ya nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ili kufungua milango ya biashara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa Kikao cha ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa (hayupo pichani), kando ya Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria.

Dkt. Nchemba alitumia mazungumzo hayo kuzitaka Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kuangalia uwezekano wa kuweka riba nafuu kwenye mikopo inayotolewa kupitia madirisha ya ujenzi wa miundombinu ili nchi za Afrika ziweze kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji hatua itakayochangia kukamilisha miradi husika kwa wakati.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao, kilichofanyika kando ya Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Abuja,Nigeria).

Benki ya Dunia ni mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo imewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo pamoja na kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news