1. Kuanzia mwaka wa masomo 2023/2024 Serikali ilianza kutoka mikopo kwa wanafunzi wenye sifa wanasoma stashahada (Diploma) za kipaumbele kwa Taifa ambazo zinatajwa kwa kina katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Stashahada kwa 2024/2025’ unaopatikana katika heslb.go.tz;
2.Hivyo, katika mwaka wa masomo 2024/2025 unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2024, wanafunzi wenye sifa wanaendelea kuomba ili hatimaye kuwezeshwa kusoma kozi za stashahada;
3. Kwa kuwa dirisha la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao linakaribia kufungwa, (Agosti 31, 2024) tunawakumbusha kuwa stashahada zinazopewa kipaumbele ni kwenye maeneo yafuatayo:
a. Health and Allied Sciences
b. Education and Vocational Training
c. Transport and Logistics
d. Energy Engineering, Mining and Earth Science
e. Agriculture and Livestock
f. Kozi nyinginezo
‘Energy Engineering’, ‘Mining & Earth Science’, na ‘Agriculture & Livestock’ ambazo hazikutajwa kwenye kipengele cha D na E kama tangazo linavyoonesha, wanaruhusiwa kuomba mkopo na watapimwa uhitaji wao wa mkopo kupitia kingámua uwezo.
KUMBUKA: Ili kuomba mkopo, tembelea: olas.heslb.go.tz/olams/pre-appl…
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Jumatano, Agosti 28, 2024