NJOMBE-Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri amefanya ziara mkoani Njombe na kutembelea mradi wa AvoAfrica mjini Makambako.
AvoAfrica, mwekezaji mkubwa katika usindikaji wa parachichi, sasa inapanua uwekezaji kwa kujenga kiwanda cha kusindika mafuta ya parachichi.
Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 100,000 za parachichi kwa mwaka. Mashine zinatarajiwa kufika mwezi Novemba mwaka huu.