BoT yaongoza kikao cha mashauriano Dar

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeongoza kikao cha mashauriano kuhusu uidhinishaji wa ripoti ya uchambuzi wa vihatarishi vinavyotokana na kuongezeka kwa utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi katika sekta ya mabenki.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha wa BoT, Bw. Sadati Musa, amesema Tanzania ipo katika mchakato wa kutekeleza Mpango wa Kikosi Kazi cha Shirika la Kimataifa la Kupambana na Uhalifu wa kifedha (Financial Action Task Force) ambao unawataka kuiimarisha na kuilinda Sekta ya Fedha dhidi ya uhalifu wa kifedha.
“Mpango kazi wa FATF unatutaka tufanye uchambuzi wa vihatarishi vinavyotokana na kuongezeka kwa utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi kwa ajili ya kuelewa vihatarishi vilivyopo ili kukabili uhalifu huo,” amesema mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa msingi wa kikao hiki unatokana na tathmini iliyofanywa na BoT kwa kushirikiana na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) na wadau wengine kuhusiana na vihatarishi vinavyotokana na kuongezeka kwa utakatishaji fedha.
“Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na FIU na wadau wengine ilifanya tathmini ya vihatarishi vinavyotokana na kuongezeka kwa utakatishaji fedha kwenye sekta ya mabenki. Ili kukamilisha zoezi hilo BoT imeaandaa kikao hiki kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha ripoti hii,” amesema Bw. Sadati.

Kikao hicho kimeanza leo Jumatatu tarehe 5 hadi 7 Agosti, 2024 katika ofisi za makao makuu ndogo ya Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news