ZANZIBAR-Benki Kuu ya Tanzania imeendesha mafunzo kwa wasanii wa Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na wakufunzi wa sanaa wanaoshiriki katika Tamasha la Kizimkazi visiwani Zanzibar.
Mafunzo hayo yamelenga kuwapa uelewa juu ya majukumu ya Benki Kuu, ikiwa ni pamoja na utambuzi wa alama za usalama zilizopo kwenye noti za Tanzania.
Pia, mafunzo hayo yamewapa washiriki ujuzi wa namna bora ya kuhifadhi noti na sarafu ili kuongeza muda wa matumizi yake.