DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo kuhusu kazi zake kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari John Merlini walipofanya ziara katika ofisi za makao makuu ya BoT jijini Dodoma. Katika ziara hiyo, wanafunzi wamepata fursa ya kujifunza kuhusu majukumu ya BoT katika kusimamia sera ya fedha, kudhibiti kiwango cha mfumuko wa bei, na kuhakikisha uthabiti wa uchumi wa nchi. Vilevile, wanafunzi hao wamepewa elimu kuhusu alama za usalama zinazowezesha kutambua noti halali za Tanzania pamoja na njia sahihi za utunzaji wa noti na sarafu ili kuhakikisha zinaendelea kudumu katika mzunguko wa fedha kwa muda mrefu. Mafunzo hayo yameendeshwa na Mchumi kutoka Tawi la BoT Dodoma, Bi. Regina Mwaipopo pamoja na Afisa Mwandamizi wa Benki, Bw. Atufigwege Mwakabalula.