Breaking News:Rais Dkt.Samia ateua mawaziri na viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 14,2024 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:-

A: Uteuzi wa Mawaziri

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria;

Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu);

Aidha, Mhe. Jenista Joackim Mhagama (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); na

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Chana alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, anachukua nafasi ya Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.

B: Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Jaji wa Mahakama ya Rufani

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua, Bw. Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani;

Bw. Samwel Maneno ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Maneno alikuwa Msaidizi wa Rais, Sheria.

Bw. Maneno anachukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Sheria na Mikataba; na

Naye, Dkt. Ally Saleh Possi ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Possi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.

C: Uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa na Naibu Makatibu Wakuu

CP. Salum Hamduni ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huu, CP. Hamduni alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), anachukua nafasi ya Prof. Siza Tumbo ambaye amerejea Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA);

Bw. Ismail Rumatila ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Rumatila alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);

Bw. Atupele Webster Mwambene ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya elimu.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwambene alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;

Bw. Abdul Rajab Mhinte ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mhinte alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais-Ikulu; na

Bw. Methusela Stephen Ntonda ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Ntonda alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais-Ikulu.

D: Uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu

Dkt. Grace Elias Magembe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya afya;

Dkt. Charles Enock Msonde amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi;

Dkt. Wilson Mahera Charles amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya elimu ya msingi na sekondari;

Prof. Daniel Elius Mushi amehamishwa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya sayansi na elimu ya juu;

Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amehamishwa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria;

Dkt. Khatibu Malimi Kazungu amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu.

Aidha, Dkt. James Peter Mataragio atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya petroli na gesi;

Bw. Ludovick James Nduhiye amehamishwa kutoka Wizara ya Ujenzi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi;

Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji.

Aidha, Dkt. Hussein Mohamed Omar atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula.

E: Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya

Kanali Maulid Hassan Surumbu amehamishwa kutoka Wilaya ya Tarime kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali. Kanali Sulumbu anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Denis Filangali Mwila ambaye amepangiwa majukumu mengine;

Meja Edward Flowin Gowele amehamishwa kutoka Wilaya ya Rufiji kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime;

Bw. James Wilbert Kaji amehamishwa kutoka Wilaya ya Tanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi;

Bw. Zephania Stephan Sumaye amehamishwa kutoka Wilaya ya Moshi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto;

Bw. Japhari Kubecha Mghamba amehamishwa kutoka Wilaya ya Lushoto kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga;

Bi. Rebecca Sanga Msemwa amehamishwa kutoka Wilaya ya Morogoro kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi;

Bi. Gift Isaya Msuya amehamishwa kutoka Wilaya ya Bahi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani; na

Bw. Mussa Ramadhani Kilakala amehamishwa kutoka Wilaya Pangani kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

F: Uteuzi wa Katibu Tawala wa Wilaya

Bi. Proscovia Jaka Mwambi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba.

G: Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri

Bw. John Lipes Kayombo amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha;

Bw. Juma Hamsini Seph amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga;

Bw. Fredrick Damas Sagamiko amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma;

Bw. Elihuruma Mabelya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam;

Bw. Jomary Mrisho Satura amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke;

Bi. Joanfaith John Kataraia amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida;

Bw. Jeshi Godfrey Lupembe amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro;

Bw. Khamis Jaaphar Katimba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi;

Bi. Rose Robert Manumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala;

Bw. Stephen Edward Katemba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali;

Bw. Missana Kalela Kwangura amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga;

Bi. Happines Joachim Msanga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe; na

Dkt. Amon David Mkoga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

H: Uteuzi wa Wakuu wa Taasisi

Bw. Crispin Chalamila ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Chalamila alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;

CPA. Moremi Andrea Marwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, CPA. Marwa alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza (SHIMA); na

Dkt. Irene Isaka ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uapisho wa Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Katibu Tawala wa Mkoa na Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kesho tarehe 15 Agosti, 2024 saa 8.00 mchana.






Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news