Carlo Ancelotti awalaumu wachezaji Real Madrid sare ya 1-1 dhidi ya Mallorca

NA DIRAMAKINI

SARE ya bao 1-1 kati ya Real Madrid dhidi ya Mallorca umemtia hasira Kocha Mkuu, Carlo Ancelotti huku akiwaelekezea lawama wachezaji wake.
Kocha Mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.(Picha na Reuters).

Ni kupitia mtanange uliopigwa Agosti 18,2024 huko Mallorca Son Moix Stadium uliopo Palma de Mallorca, Balearic Islands nchini Uhispania.

Kupitia michuano hiyo ya La Liga, Ancelotti amewataka wachezaji wake kujikita katika kujilinda na kushambulia zaidi.

Real Madrid ilionekana kukosa uwiano walipokuwa wakianza kutetea ubingwa wa LaLiga, hivyo kuambulia sare hiyo.

Dakika ya 13' katika mtanange huo,Rodrygo Silva de Goes (Rodrygo) ndiye aliyeanza kuandika bao la kwanza kwa klabu hiyo ikiwa ugenini.

Bao hilo lilidumu kipindi chote cha dakika 45 ambapo, kipindi cha pili dakika ya 53, Vedat Muriqi aliwasawazishia Mallorca.

“Tunaporudisha mpira nyuma, lazima tufikirie vyote kwa pamoja, unaweza kufikiria kuwa ni shida ya mshambuliaji, lakini inaweza kuwa shida ya safu ya ulinzi, au ya viungo.

“Sio tatizo la mmoja, wawili au watatu. Ni tatizo la timu ambayo katika mechi hii haikuelewa ni mambo ya msingi. Mallorca walicheza mchezo mzuri kwa kujilinda, bora kuliko sisi. Sare ni matokeo sahihi.”

Pengine kilichomsikitisha zaidi, Kocha Mkuu Ancelotti ni pamoja na Ferland Sinna Mendy kulimwa kadi nyekundu dakika ya 90'.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news