ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema chama hicho kipo imara na kinaendelea kujipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Agosti 26, 2024, wakati alipokutana na Ujumbe wa Umoja wa Madiwani wa CCM Tanzania, ukiongozwa na Katibu wake,Hilda Augustino Kadunda, uliofika Ikulu kuonana naye.
Aidha, ameeleza kuwa CCM haitasita kuwaeleza wananchi mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, na ujenzi wa masoko ili wananchi waweze kuyafahamu mafanikio hayo.
Naye Katibu wa Umoja wa Madiwani wa CCM Tanzania,Hilda Augustino Kadunda, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya kuiletea maendeleo Zanzibar na wananchi wake.
Ameeleza kuwa, utekelezaji wa Ilani 2020-2025 kwa CCM Zanzibar ni wa kuigwa mfano kwani umevuka malengo yaliyoainishwa.