CCM itaendelea kuhubiri amani,umoja na mshikamano-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea na msingi yake ya kudumu ya kujenga Amani, Umoja na Mshikamano na kuwahimiza wana CCM kuwa wastahamili wakati huu kuelekea uchaguzi ujao.Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Agosti 12, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Wadi, Tawi, Jimbo, Wilaya na Mkoa za Mkoa wa Kusini kichama katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein, Tunguu.
Aidha,Dkt.Mwinyi amewanasihi viongozi wa Vyama vya Siasa kuacha kuhubiri Siasa za chuki na badala yake kuhubiri Amani kwa dhamira ya kuimarisha Amani ya nchi.

Halikadhalika Dkt.Mwinyi amesema, Chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kwa asilimia mia moja katika utekelezaji wa Ilani na kuwahimiza wananchi kuunga mkono hatua hiyo.
Pia ameeleza kuwa, Serikali bado ina mpango wa kujenga barabara ya kisasa kuanzia Tunguu hadi Makunduchi yenye urefu wa takriban kilomita 43. Barabara hiyo itakuwa ya njia nne na yote itafungwa taa.

Kwa upande mwingine Dkt.Mwinyi amewasisitiza wana CCM kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura ili kuwa na sifa ya kushiriki Uchaguzi mkuu mwakani na kukihakikishia Chama cha Mapinduzi Ushindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news