Chuo Kikuu cha Mzumbe,University of Bonn wasaini hati ya makubaliano na ushirikiano

MOROGORO-Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema Mzumbe iko tayari kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi katika kubadilishana uzoefu katika maeneo ya taaluma na tafiti.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (kulia) na Prof. Detflef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn (kushoto) wakitia Saini ya Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn.

Prof. Mwegoha amesema hayo wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn yanalolenga kuimarisha uhusiano wa kitaaluma na kuboresha ubora wa elimu, utafiti na ubunifu baina ya vyuo hivyo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn kwenye Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn.
Awali, Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn amesema ni fursa kwao kuimarisha ushirikiano utakaoleta tija baina vyuo hivyo kwa kuinua viwango vya elimu ya juu na utafiti katika nyanja mbalimbali huku ukihimiza uvumbuzi na ubunifu.

Makubaliano hayo ya ushirikiano yanaelekeza ushiriki wa Chuo Kikuu Mzumbe katika miradi ya utafiti na kuboresha mitaala ili kukidhi mahitaji ya soko ya ajira kimataifa.
Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn.

Pia, ushirikiano huo utaleta fursa za semina, warsha na kongamano za kitaaluma zinazolenga kujadili changamoto na mbinu bora za kuboresha elimu na utafiti.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (kulia) akikabidhi zawadi ya kumbukumbu kwa Prof. Detflef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn (kushoto) baada ya Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn.

Hati ya makubaliano baina ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo cha Bonn ni ya miaka mitano kufuatia kukamilika kwa awamu ya kwanza ambapo wanataaluma wamenufaika na fursa za masomo na tafiti katika nyanja za taaluma na tafiti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news