ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth and Community Rehabilitation (YCR) imeongoza kampeni maalum ya uokotaji sindano ambazo zimeshatumika na waraibu wa dawa za kulevya kwenye mazingira hatarishi jijini Arusha.
Zoezi hilo maalum limefanyika Darajani, Ngarenaro na Ungalimited likilenga kuweka jamii salama dhidi ya madhara yatokanayo na utupaji hovyo wa sindano ambazo zimeshatumika;
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)