DCEA yashiriki mkutano wa Kimataifa wa Jumuiya ya Wataalamu wa Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya

ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imeshiriki mkutano wa Jumuiya ya Wataalamu wa Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya kwa nchi za Afrika uliofanyika jijini Arusha Agosti 21 na Agosti 22,2024.
Mkutano huo umezikutanisha nchi wanachama wa ISSUP upande wa Bara la Afrika ili kujadili masuala muhimu yanayohusu namna ya kuboresha tiba na huduma za utengamao kwa waraibu wa dawa za kulevya kwa kutumia njia sahihi na zilizothibitishwa kisayansi.
Aidha, mkutano huo umetoa fursa ya wataalam kubadilishana uzoefu, kushirikishana matokeo ya tafiti mbalimbali za tiba kwa waraibu pamoja na kutoa fursa ya mafunzo kwa wataalamu wa tiba kwa waraibu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news