MTWARA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Kanda ya Pwani imetoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya katika shule za sekondari na msingi mkoani Mtwara.
Shule zilizofikiwa ni Lukuledi, Chiwale, Nangaya, Mtandi, Chanikangu, Ndanda, Nanyindwa, Mrawishi, Njenga, Lukuledi, Chiwale, Ufukoni na Lilala.
Pamoja na elimu hiyo washiriki wote wamehimizwa kutojihusisha na matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya ili kuwa na jamii isiyojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya. Katika hatua nyingine, walimu wa shule hizo kwa ujumla wameishukuru Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya nchini (DCEA) kwa elimu hiyo na kuomba iwe endelevu.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)