DCP Nyambabe akabidhi Bendera kwa askari wa kike wanaokwenda kushiriki mafunzo ya Dunia nchini Marekani

NA ABEL PAUL

NAIBU Kamishna wa Polisi kutoka Kitengo cha Udhibiti Makosa yanayovuka Mipaka, DCP Daniel Nyambabe amewakabidhi askari wa kike Bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda nchini Marekani kushiriki mafunzo kwa askari wa kike duniani katika Jimbo la Chicago kuanzia Septemba 01 hadi 05, mwaka huu.
DCP Nyambabe akikabidhi bendera hiyo leo Agosti 26,2024 Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam amesema, askari hao wanakwenda kuhudhuria mafunzo hayo ya Dunia ambayo yanahusisha askari wa kike na wasimamizi wa sheria ambapo amewasisitiza kuzingatia mafunzo nchini Marekani.

Ameongeza kuwa, Jeshi la Polisi linaamini kuwa mafunzo wanayokwenda kuyapata yataleta chachu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaamini kuwa washiriki hao ni kielelezo kizuri cha nchi ambapo amewataka kuwa na nidhamu kipindi chote cha mafunzo.

Aidha, ameeleza kuwa kuwa ushiriki wa askari wa Jeshi la Polisi katika mafunzo hayo ya Dunia ni uwakilishi wa Nchi ambapo amewataka askari hao Kwenda kulinda na kutunza taswira nzuri ya nchi iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wa nchi hii.

Sambamba na hilo DCP Nyambabe amewaomba maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutumia fursa ya mafunzo hayo kutengeneza mtandao wa mawasiliano ambayo yatasaidia katika mapambano dhidi ya uhalifu na kumjengea uwezo askari mmoja mmoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news