Dereva aliyesababisha ajali ajisalimisha polisi

SHINYANGA-Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limemchukulia hatua dereva wa kampuni ya Happy Nation aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T402 EFH lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam.
Ni aliyesababisha ajali iliyopelekea vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa mnamo Agosti 19,mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari Agosti 21, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amesema kuwa,kupitia kikosi cha usalama barabarani jumla ya makosa 3,084 yamekamatwa pamoja na kufungiwa leseni ya udereva madereva wawili kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya watu watatu.

Kamanda Magomi amebainisha kukamatwa kwa gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T886 DCU ikiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi bunda mbili zenye uzito wa gramu 400.

Aidha,Kamanda Magomi amesema jumla ya kesi 20 zimepatiwa ufumbuzi mahakamani ikiwemo watu wawili kuhukumiwa kunyongea hadi kufa kwa makosa ya mauaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news