ZANZIBAR-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Mhe. Doto Biteko amemkabidhi Cheti cha Udhamini Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),Mhandisi Hassan Saidy wakati wa Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyikia Kizimkazi, Mkoa wa Unguja Kusini Zanzibar.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Mhe. Doto Biteko akimkabidhi Cheti cha Udhamini Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),Mhandisi Hassan Saidy wakati wa Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyikia Kizimkazi, Mkoa wa Unguja Kusini Zanzibar.
REA ni miongoni mwa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati zilizodhamini Kongamano hilo la Nishati Safi ya Kupikia lililobeba kaulimbiu ya 'Upishi Salama kwa Afya ya Mpishi na kwa Maendeleo ya Jamii'.
Katika kongamano hilo, REA ilipata fursa ya kushiriki mdahalo ambapo Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mha. Advera Mwijage alizungumzia Upatikanaji wa Fedha katika kuendeleza Nishati Safi ya Kupikia.