Dkt.Biteko ashiriki kikao cha mawaziri wa Nishati nchini Uganda

KAMPALA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto BIteko leo tarehe 15 Agosti, 2024 ameshiriki kikao cha 19 cha pamoja cha Mawaziri wa Nishati ambao ni Wanachama wa Umoja wa soko la pamoja la kuuziana umeme na kuimarisha mifumo ya Gridi ya EAPP (Eastern Africa Power Pool) unaofanyika nchini Uganda.
Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo kupitisha mabadiliko ya mikataba ya uongozi wa EAPP, kuridhia kanuni za uanzishwaji wa kitengo kinachojitegemea cha kusimamia soko la biashara ya umeme kwa nchi wanachama (Marketing and Trading unit) na kuridhia kanuni na taratibu za uendeshaji wa vikao vya Baraza la Mawaziri, Makatibu wakuu, na kamati ya uongozi.
Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mha. Gissima Nyamo-Hanga, Naibu Mkurugenzi Mipango, utafiti na uwekezaji CPA Renatha Ndege, na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news