NAIROBI-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika ( US-Africa Nuclear Energy Summit).

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameambatana na Watendaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.