DODOMA-Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF), Dkt.Irene Isaka ameripoti rasmi katika Ofisi za Makao Makuu jijini Dodoma leo Agosti 19,2024.
Akizungumza na Menejimenti ya Mfuko na Watumishi, ameeleza jinsi ambavyo Serikali ilivyo na matarajio makubwa hasa katika utatuzi wa kero za wananchi kuhusu Bima ya Afya.