Dkt.Mwinyi azima zote,awasha kijani Zanzibar

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahakishia Vijana kuwa Serikali imekusudia fungu la fedha ili kuwawezesha katika Elimu , Ajira na Uwezeshaji.
Rais Mwinyi aliyasema hayo Agosti 10, 2024 katika Uwanja wa New Complex Amaan wakati wa alipozindua kampeni ya kijana kijani ya Tunazima zote Tunawasha kijani iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa katika kuwainua Vijana Serikali iweka mkazo katika maeneo matatu ambayo Ongezeko la Ajira, fungu la Mikopo kuwafikia vijana na nafasi za uteuzi za Uongozi.

Dkt.Mwinyi amewahimiza vijana kujipanga na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za Uongozi katika Vyombo vya Maamuzi na Serikali itawaunga mkono.
Ametumia fursa hiyo kuvishauri Vyama Upinzani kujifunza kwa Uvccm namna Bora ya kufanya Siasa na kuupongeza Umoja wa vijana kwa kazi nzuri.
Kwa upande mwingine, Dkt.Mwinyi amewapokea Wanachama 368 kutoka Vyama vya ACT Wazalendo na CUF waliojiunga na CCM wakiongozwa na Ndugu Ahmed Omar aliyewahi kuwa Msaidizi wa Maalim Seif Shariff Hamad na Juma Duni Haji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news