ARUSHA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amewataka viongozi wa ofisi hiyo kufanya kazi katika ubora na weledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwahudumia Watanzania.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akihitimisha kikao cha Mazingativu (Retreat) kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake jijini Arusha leo Agosti 1,2024.
Ameyasema hayo mapema leo Agosti 1, 2024 Jijini Arusha alipohitimisha kikao za mazingativu (Retreat) kilichohusisha viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Menejimenti, Watumishi na taasisi zilicho chini ya Ofisi hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akigawa vyeti kwa viongozi wakati wa kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika jijini Arusha leo Agosti 1,2024.
Dkt. Yonazi alisema kuwa ana imani kubwa kwa watumishi na viongozi wa Ofisi hiyo kuwa watakuwa ni watumishi wenye thamani na utulivu na wenye nia ya kuwatumikia Watanzania kwa weledi na moyo thabiti.
“Sisi hapa wengi ni viongozi, watu wa chini yetu ndo wametuwezesha kuwa viongozi hivyo tumesiweke mazingira magumu kwa waliyopo chini yetu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.”
Awali akizunguza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Mipango na Bajeti kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Eleuter Kihwele amesema mafunzo hayo yalishafanyika mwaka 2023 na yamesaidia sana katika kuboresha utendaji kazi na kusaidia kuimarisha umoja kwa kuwaleta pamoja watumishi wote.
Mwezeshaji wa mada inayohusu mfumo wa maisha na nidhamu ya vyakula,Dkt. Fredrik Lazaro Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili akitoa mada katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika jijini Arusha leo Agosti 1,2024.
Sehemu ya Washiriki katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika jijini Arusha leo Agosti 1,2024.
Ameongezea kuwa, utendaji wa pamoja katika maana ya viongozi na watumishi kukaa pamoja kujadili pamoja namna ya kuleta Tija katika uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa shughuli za Serikali unachochea ufanisi kazini na kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.