Elimu ya Fedha yawafikia wananchi Morogoro, ombi latolewa

NA RAMADHAN KISSIMBA
WF

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John amewaomba watalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na sekta ya fedha nchini kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hasa watumishi wa umma zinazotokana na upatikanaji wa huduma za fedha zisizo rasmi.
Wananchi wa Halmashauri ya Morogoro Mjini wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa na wataalam wa masuala ya fedha kutoka Wizara ya Fedha na Washirika wa sekta ya fedha nchini katika ukumbi wa Mbaraka Mwinshee Mjini Morogoro.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha – Morogoro).

Bi. Ruth ameyasema hayo wakati Timu ya program maalum ya elimu ya fedha kwa umma kutoka Wizara ya Fedha na washirika kutoka sekta ya fedha nchini walipofika ofisini kwake kabla ya elimu hiyo kutolewa kwa wakazi wa Morogoro mjini.

Bi. Ruth alisema kuwa suala la mikopo isiyofuata taratibu limekuwa na changamoto nyingi sana sio kwa wajasiriamali pekee bali hata kwa Watumishi wa Umma hii inatokana na uhitaji wa fedha maana kila mtu ana uhitaji wake.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John akizungumza na Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Fedha na washirika wa sekta ya fedha nchini walipofika ofisini kwake katika muendelezo wa utoaji elimu ya fedha kwa umma.

‘’Changamoto tunazipata sana hadi kwa watumishi wa umma hususan walimu ambao wanaingia kwenye changamoto hiyo kwa sababu kila mtu ana uhitaji wake, na anapopata shida haaangalii kitu gani kipo mbele yake ambacho kitamletea madhara,’’amesema Bi. Ruth.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya akiwaeleza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mjini namna bora ya kuepukana na mikopo isiyo rasmi (mikopo umiza) wakati wa program maalum ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa wananchi hao katika ukumbi wa Mbaraka Mwinshee.

Bi. Ruth aliongeza kuwa, kumekuwa na watoa huduma wengi wanaotoza riba kubwa ambayo wakati mwingine inazidi kiasi cha mkopo na Taasisi nyingi kati ya hizo hazijasajiliwa na wakopeshaji wengine wanawakopesha wananchi majumbani ambapo ni kinyume na utaratibu.
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw Ramadhani Myonga akitoa mada kwa wananchi wa Halmashauri ya Morogoro Mjini wakati wa program maalum ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande mwingine akizungumza katika program hiyo iliyotelewa kwenye ukumbi wa Mbaraka Mwinshee Mjini Morogoro, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, alisema kuwa elimu ya fedha kwa umma ni matakwa ya Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha ambao unalenga kumlinda mlaji wa huduma ya fedha na mpango huo umetoa maelekezo ya utoaji elimu ya fedha nchini.
Mratibu wa Mifuko na Program za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Samwel Shikona akiwaeleza wananchi wa Morogoro fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia Baraza hilo wakati wa program maalum ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa wananchi wa halmashauri hiyo.

Bw. Kibakaya aliongeza kuwa mpango huo wa miaka 10 ambao utekelezaji wake umeanza mwaka 2020/21, Wizara imejiwekea malengo hadi kufikia mwaka 2025 kuhakikisha asilimia 80 ya wananchi wamepata uelewa wa masuala ya fedha na waweze kuzitumia vizuri fursa zinazopatikana katika sekta ya fedha nchini.

Aidha, Bw. Kibakaya alisema kupitia mafunzo yaliyotolewa kwa wananchi wa Morogoro yatasaidia kwa watoa huduma ndogo za fedha na wanufaika wa huduma hizo kufuata sheria za huduma ndogo za fedha na kanunuzi zake kama zinavyoelekeza.
Mratibu wa Mifuko na Program za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Samwel Shikona akiwaeleza wananchi wa Morogoro fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia Baraza hilo wakati wa program maalum ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa wananchi wa halmashauri hiyo.

Serikali iliamua kutoa elimu ya fedha kwa wananchi baada ya kugundua kuwa kuna kundi kubwa la watanzania ambao hawafaidiki na huduma za fedha na hivyo kukosa fursa za kuboresha maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi na hatimaye kuchangia katika kukuza pato la Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news