Geita itajengewa jengo la Zimamoto na kupatiwa gari-Mheshimiwa Sillo

GEITA-Serikali imekihakikishia Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi Mkoa wa Geita Kuwa itatumia Shilingi Milioni 699.9 kukamilisha Ujenzi wa Jengo la Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na kupatiwa Gari la Zimamoto katika Mkoa huo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi,Dkt.Emmanuel Nchimbi aliyofanya kwenye Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri Sillo, ameyasema hayo wakati akijibu changamoto iliyoibuliwa na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu ya uwepo wa uhaba wa vitendea kazi na kutokuwa na Gari la Zimamoto na Uokoaji pamoja na kutokamilika kwa Ujenzi wa Jengo la Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapo.
Naibu Waziri Sillo, amesema Serikali itakamilisha Ujenzi wa Jengo hilo la Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita kwa kutumia gharama za fedha Shilingi 699.9 milioni ambapo mpaka sasa tayari ilishatumia zaidi ya Shilingi 285,714,000 milioni sawa na asilimia 38 na mwaka huu wa fedha wa 2024/25 tayari Serikali imetenga fedha Shilingi 414,285,000 milioni.
Kadhalika Mhe. Sillo, amesema tayari Serikali imeagiza magari ya Zimamoto na Uokoaji 150 ambayo yatasambazwa kwenye mikoa na wilaya ambazo hazina magari hayo ukiwemo mkoa huo wa Geita ambao utapatiwa gari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news