Geita wajitokeza kwa wingi uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

GEITA-Wananchi wengi wamejitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo limekamilika leo Agosti 11, 2024 mkoani Geita baada ya kufanyika kwa siku saba kuanzia Agosti 5, 2024.
Wakazi wa Mji wa Geita mkoani Geita wakiwa foleni katika moja ya vituo vya kuboreshea Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani humo kwaajili ya kuboresha taarifa zao na kujiandiskisha leo ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi hilo mkoani Geita. Zoezi hilo pia linafanyika mkoani Kagera na lilianza Agosti 5 hadi 11,2024.
Wakazi wa Mji wa Geita mkoani Geita wakiwa katika moja ya vituo vya kuboreshea Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani humo kwaajili ya kuboresha taarifa zao na kujiandiskisha leo ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi hilo mkoani Geita. Zoezi hilo pia linafanyika mkoani Kagera na lilianza Agosti 5 hadi 11,2024.

Mwandishi wetu ameshuhudia uwepo wa wananchi wengi vituoni haswa vijana ambapo kwenye baadhi ya maeneo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ililazimika kuongeza vifaa na watendaji.

Wakizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Geita Mji, Bw. Yefred Mnyenzi na Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Bi. Sarah Yohana wamesema wengi waliojitokeza ni vijana ambao wanajiandikisha kwa mara ya kwanza.
Wakazi wa Mji wa Geita mkoani Geita wakiwa katika moja ya vituo vya kuboreshea Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani humo kwaajili ya kuboresha taarifa zao na kujiandiskisha leo ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi hilo mkoani Geita. Zoezi hilo pia linafanyika mkoani Kagera na lilianza Agosti 5 hadi 11,2024.
"Kwa siku hawapungui wapiga kura 10,000 ambao wamejitokeza, kati yao wapiga kura wapya ambao wengi ni vijana ni kama 8,000 kwa siku, kwa ujumla nawapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi,” amesema Bw. Myenzi, Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Geita Mji.

Kwa upande wake, Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Bi. Sarah Yohana amesema “Wananchi wamejitokeza kwa wingi haswa vijana, maeneo yaliyokuwa na wananchi wengi zaidi ni ya Katoro, Rwemgaza na Kiziba ambapo tumeongeza vifaa na watendaji wa vituo, kwa mfano, Katoro tumeongeza BVR Kits 10 na Waandikishaji na Waendesha Vifaa vya Bayometriki 20”.
Wananchi wakijiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura. (Picha zote na INEC).

Wakizungungumza kwa nyakati tofauti wapiga kura waliojiandikisha na kuboresha taarifa zao wameishukuru INEC kwa kuboresha huduma kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa ambayo imerahisisha zoezi hilo jambo ambalo limepunguza muda wa kujiandikisha na kuboresha taarifa ambapo wameweza kupata kadi zao ndani ya dakika tatu hadi tano.

“Kwa mara ya kwanza nimeweza kupata kadi yangu hii ya mpiga kura, ambayo itaniwezesha kupiga kura kumchagua kiongozi wangu. Nashukuru kwa teknolojia iliyowekwa nimeweza kutumia takribani dakika nne hadi kupata kadi yangu ya mpiga kura,” amesema Angel Lema ambaye amefikisha miaka 18 mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news