ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Taasisi za Mabenki Yasiyo na Mipaka (Bankers Without Boundaries) kuwekeza miradi ya kipaumbele na yenye tija kwa nchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Mabenki Yasiyo na Mipaka ambayo Makao Makuu yake yapo nchini Uingereza, Bw. Matteo Scollabrino aliyefika Ikulu na ujumbe wake leo Agosti 14, 2024.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe: 14 Agosti 2024, alipokutana na Mkuu wa Taasisi ya Mabenki Yasiyo na Mipaka ambayo Makao Makuu yake yapo nchini Uingereza, Bw. Matteo Scollabrino aliyefika Ikulu na ujumbe wake.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema sekta ya Uchumi wa Buluu, Kilimo, Nishati, Miundombinu, na Afya ni sehemu ya miradi ya kipaumbele kwa Serikali na inahitaji msukumo wa ziada ili iweze kuleta tija kwa nchi.

Kikao hicho ambacho kimefanyika Ikulu Zanzibar kimehudhuriwa na watendaji wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Presidential Delivery Bureau (PDB).