Gridi ya Taifa ina umeme wa kutosha-Rais Dkt.Samia

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mfumo wa gridi ya Taifa una umeme wa kutosheleza mahitaji ya kijamii na kiuchumi.Rais Dkt.Samia ameyasema hayo leo Agosti 2, 2024 wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi.
Ameeleza kuwa, Serikali inazidi kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ambapo imejenga kituo cha kupokea na kupoza umeme wilayani Kongwa mkoani Dodoma ambacho kitaboresha pia hali ya umeme wilayani Gairo.
Ameongeza kuwa, njia ya kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupoza umeme cha Kongwa kwenda wilayani Gairo imeshakamilika.

"Mambo mengine yapo vizuri, umeme ameeleza vizuri, lakini pia Gairo ninajua mlikuwa na changamoto ya kupungua au kukatika kwa umeme.

"Tumejenga substation pale Kongwa, kuna substation ambayo itatumika mpaka Gairo kufanya umeme usikatike.
"Na kwa bahati nzuri Gridi yetu sasa ina umeme wa kutosha, na njia ya kuleta umeme huu iko tayari.

"Kwa hiyo tumejenga substation, kituo cha kupokea na kupoza umeme ili tupunguze ile kadhia ya kukatikakatika kwa umeme.
"Sasa, Gairo mna bahati, mambo yote yamefanyiwa kazi, changamoto zote zilizosemwa zinakwenda kufanyiwa kazi, yanayofanyika Gairo yanafanyika mkoa wote wa Morogoro,"amesisitiza Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news