GSM akikasirika tuna uwezo wa kununua timu yoyote hapa nchini-Ally Kamwe

NA DIRAMAKINI

MSEMAJI wa Young Africans Sports Club ya jijini Dar es Salaam,Ally Kamwe amesma mwekezaji katika klabu hiyo GSM akasirika anaweza kununua timu B ya Yanga.
Kamwe ameyasema hayo Agosti 23,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari kuelekea uzinduzi wa michuano ya CAF.

“GSM akikasirika tuna uwezo wa kununua timu yoyote hapa ikawa timu B ya Yanga, wewe unatumia bilioni 7 unapiga kelele unaita na waandishi unawaambia umetumia bilioni 7 unajua GSM katumia kiasi gani kwenye usajili ?.

“Bilioni 7 ni wachezaji wawili au watatu wa Yanga, hivi mnajua Diarra amesaini miaka mitatu alafu unazungumza kuhusu bilioni 7 mkija kupigwa tano mnaanza kusingizia watu sisi tuko level za juu tunaelekea kulipa watu bilioni.

“Msimu huu tuna timu bora kuliko muda wowote ule, tunayo timu tishio sio tu ndani ya Tanzania hadi nje ya mipaka ya Tanzania.

"Nitashangaa kusikia watu wanasema Mzize inabidi atoke ili akakue zaidi, lakini watu hao hao hawaangalii tulipomtoa Mzize, Wananchi tupuuze maneno yao kwani lengo lao wanataka kutuvuruga.

"Nawahakikisha Clement Mzize, bado yupo sana Yanga. Kama ndoto zenu ni Mzize aondoke kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu, chini ya Injinia Hersi hawezi kuondoka Yanga.

"Tunayo nguvu ya ushawishi na nguvu ya kiuchumi. Tuna wachezaji bora na watabaki kuwa bora ndani ya Yanga. Shida yenu hamuamini kama Yanga imekuwa klabu bora na kubwa Afrika.

“Tumeweka rekodi ya kwanza ya klabu kufanya mkutano mkubwa wa CAF, tunazungumzia ukumbi na sio chumba. Jambo hili ni heshima kubwa sana kwetu, kimsingi tumeheshimisha soka la Tanzania.

“Tunawaalika sana Chamazi kutakuwa na burudani kubwa sana, tutakuwa na DJ Ally B pamoja na wasanii mbalimbali ambao tutawatangaza.

"Kwa hiyo tujitahidi kadiri iwezekanavyo tuwahi kukata tiketi mapema sana,”amesema Ally Kamwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news