Haji Manara kupangiwa majukumu mengine Young Africans Sports Club

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Young Africans Sports Club ya jijini Dar es Salaam umesema, unatarajia kumpangia majukumu mengine Msemaji wao, Haji Manara.
Hayo yamebainishwa Agosti 21,2024 na Rais wa klabu hiyo,Mhandisi Hersi Said kupitia mahojiano maalum na Wasafi Media.

“Haji Manara kwa sasa ni mwanachama hai wa Yanga, tunaangalia majukumu mapya ya kumpatia klabuni. Ali Kamwe bado yupo kwenye nafasi yake ile ile na Manara atapatiwa nafasi nyingine.”

Katika hatua nyingine, Mhandisi Said ameendelea kutambua na kuthamini kipaji cha aliyekuwa mchezaji wa Yanga SC ambaye kwa sasa yupo Azam FC,Feisal Salum Abdalla (Fei Toto).

“Feisal ni bora ya wachezaji bora tulio nao kwenye ligi yetu, mimi ninamjua binafsi ni kijana mzuri, kwenye maisha yangu sijawahi kuwa na shinda na Feisal na yeye analijua hilo.

“Sitaki kuhukumu yaliyopita mimi ni kiongozi wa mpira tunamuhitaji kwenye maendeleo ya Taifa letu, tunamuhitaji kwenye vilabu vyetu, tunamuombea Mungu afanye vizuri ni hazina kwenye timu yetu,” amesema Rais huyo wa Yanga SC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news