Hakuna anayeachwa nyuma Zanzibar,Rais Dkt.Mwinyi aendelea kutekeleza kila sekta

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa kukifanya kilimo biashara chenye tija kwa kuimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi kwa mlaji.Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Julai 3,2024 alipofungua maonesho ya saba ya kilimo ya Nane Nane Zanzibar katika viwanja vya Dole, Kizimbani Mkoa wa Mjini.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaanzisha vituo maalum kila wilaya kuhamasisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima na wafugaji nchini.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali inatarajia kutekeleza mradi mkubwa wa mageuzi wa uzalishaji wa wafugaji wa maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo ambao utazingatia mabadiliko ya tabia nchi yenye gharama za shilingi bilioni 7.5.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mifugo kwa kujiajiri, pia amewahimiza wajifunze mbinu bora za kilimo na ufugaji kupitia maonesho ya kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news