Israel Mwenda aondoka Simba SC

DAR-Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam imethibitisha kuridhia ombi la mchezaji,Israel Mwenda kuondoka klabuni hapo baada ya nyota huyo kudai kuwa amepata timu nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo,Israel Mwenda alisaini mkataba mpya wa miaka miwili, lakini kabla ya kuanza kuutumikia, aliandika barua ya kuondoka kwa madai amepata timu sehemu nyingine ya kuichezea.

“Simba kwa kujali na kuheshimu maslahi ya mchezaji ilimpa sharti la kurejesha fedha zote na tayari amerejesha. Simba ina thamini mchango wa Israel katika miaka yote mitatu aliyodumu nasi.

“Uongozi wa klabu unamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya ya soka.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news