DAR-Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi leo Agosti 18, 2024 jijini Dar Es Salaam ameongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe leo Agosti 18,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Msajili.
Kikao hicho mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kimehudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akiongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo Agosti 18,2024 jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi akichangia jambo katika kikao cha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na wadau leo Agosti 18,2024 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini akichangia jambo katika kikao cha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na wadau mbalimbali leo Agosti 18,2025 jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mheshimiwa Freeman Mbowe (kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi wakifuatilia majadiliano katika kikao hicho cha wadau.
Baadhi ya viongozi wakuu wa vyama hivyo walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha CUF, ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD kwa sasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, ndugu Dorothy Semu, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na ndugu Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi akichangia jambo katika kikao cha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na wadau leo Agosti 18,2024 jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (katikati) akisisitiza jambo katika kikao hicho na wadau.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mheshimiwa Freeman Mbowe (kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.
Upande wa Serikali, uliwakilishwa na Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.