DODOMA-Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt.Mathayo Mathayo amepongeza maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Madini awamu ya pili kwa juhudi mbalimbali zinazofanyika na kupelekea kufikisha asilimia 84.4 ya ujenzi katika mji wa Serikali Mtumba.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu, Festus Mbwilo amesema mpaka kufikia Agosti 2, 2024 utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo la ghorofa tano ulifikia asilimia 84.4 na sehemu iliyobakia ni asilimia 15.6.
Awali, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa utekelezaji wa mkataba ulikuwa miezi 18 lakini kutokana na changamoto mbalimbali mkandarasi hakuweza kukamilisha kwa wakati ambapo tarehe ya mkataba ya awali kukamilisha jengo ilikuwa Aprili 14, 2023.

Ollal ameongeza kuwa changamoto nyingine ni kuchelewa kwa vifaa kulikosababishwa na upungufu wa fedha za kigeni katika manunuzi nje ya nchi.