Karoti nyeupe ambayo ni kubwa kuliko muhogo inapatikana Maonesho ya Nanenane

DODOMA-Katika kupata hamasa za aina mbalimbali za mazao yanayopatikana kwenye vitalu vya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 yaliyoanza tarehe 1 Agosti 2024, wananchi wana fursa ya kujifunza na kupata taarifa zaidi kuhusu zao la karoti nyeupe ambayo ni kubwa kuliko muhogo.
Zao hilo linapatikana katika Banda la Dodoma Jiji ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu ya kanuni bora za zao la Karoti nyeupe, kwa watakaotembelea Maonesho ya Nane Nane 2024 katika fursa za biashara, kujifunza bunifu na teknolojia za kisasa za mazao na kubadilishana uzoefu.

Akiongea na wananchi waliotembelea eneo hilo hivi karibuni,Afisa Lishe Idara ya Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi. Plaxeda Kashaija emesema kuwa zao hilo wengi hawalifahamu na hufaa kwa lishe na biashara.

"Tumelileta hapa kwa makusudi ili watu wa Dodoma waone kuna fursa katika zao la karoti nyeupe kwa kuwa ni zao linalostawi kwa muda mfupi na kukomaa kwa siku 45,” ameeleza Bi. Kashaija na kuongeza kuwa ni zao lenye uhitaji wa eneo dogo ata kwa kilimo cha majumbani, ambapo mavuno yake ni mengi.

Ameongeza kuwa, karoti nyeupe ina uwezo wa kustahimili visumbufu vya mimea haihitaji kupuliziwa viuatilifu mara kwa mara na zao hilo linaliwa majani pamoja na kiazi chake katika Supu, Saladi pamoja na mboga, ina virutubisho vya kutosha kama ilivyo kwa mboga zingine za majani na matunda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news