Katoro kupatiwa Wilaya ya Kipolisi, kujengewa kituo cha polisi

GEITA-Serikali imesema itaupatia Mji mdogo wa Katoro Mkoa wa Geita Wilaya ya Kipolisi na kuujengea Kituo kipya cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya ili kuimarisha Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa mkoani Geita.
Naibu Waziri Sillo, amesema sababu za kupeleka hitajio hilo ni kutokana na Mji wa Katoro wenye watu zaidi ya laki tatu kukua kibiashara na kiuchumi kwa kasi.

"Kituo cha Polisi kilichopo kipo katikati ya makazi ya watu na maeneo ya biashara habari njema ni kwamba IGP alituma timu yake hapa walishafanya tathimini hivyo mnajengewa Kituo kipya cha kisasa na mnapatiwa Wilaya ya Kipolisi hapa Katoro."
Aidha, Sillo amewahimiza Polisi kata nchini kuendelea kutoa elimu ya Polisi jamii kwa Wananchi na Viongozi wa Serikali za mitaa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na kutokomeza uharifu unaojitokeza maeneo mbalimbali ikiwemo wizi wa mifugo unaotajwa kuwepo kwa wingi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
"Wananchi mnapata taarifa za wezi, mnakaa nazo na wengine kuishi nao naomba toeni taarifa kwa Jeshi la Polisi ili sheria ichukue mkondo wake,"alisema Mhe. Sillo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news