Kigogo kutoka Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ajitosa Ubunge wa Afrika Mashariki

DAR-Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Saulo Mali amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Saulo Mali akielekea kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Kada huyo wa CCM ambaye kitaaluma ni mwalimu, amechukua fomu hiyo mapema leo Agosti 12,2024 katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya mlchama, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Saulo Mali akielekea kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo,Grace amesema ana dhamira ya dhati ya kuwania kiti hicho kilichoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dkt.Shogo Mlozi, ambaye aliyefariki dunia Juni,mwaka huu.

Grace amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na chama kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwania nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Saulo Mali akiongea na waandishi wa habari baada ya kuhusu dhamira yake ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Saulo Mali baada ya kuwasili kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Amesema, kipaumbele chake kikubwa atakapopata nafasi hiyo ya kuliwakilisha taifa katika Bunge la Afrika Mashariki ni elimu.

“Pia kuwasaidia vijana waliosoma, lakini hawana ajira kwa kuwaunganisha na fursa,”amesema.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Saulo Mali alipowasili kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA).

Amewataka watanzania kumuunga mkono Rais Dkt. Samia katika sekta mbalimbali alizowekeza.

“Tumuunge mkono rais katika sekta ambazo amewekeza kwa ukubwa.Taaluma yangu mimi ni mwalimu na kipaumbele changu katuka kumuunga mkono ni katika,”amesema ambapo CCM jana imeanza kutoa fomu hizo nchini kote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news