NA DIRAMAKINI
MKUU wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (The Bank of Tanzania Academy (BOT-AC), Dkt.Nicas Yabu katika mahojiano na Meneja Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Vick Msina amefafanua kwa kina kuhusu historia ya chuo hicho na majukumu yake.
"Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania kilianzishwa mwaka 1991 na kwa wakati huo kilikuwa ni kwa makusudi ya kuwafundisha wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania, lakini pia wafanyakazi wa Sekta ya Fedha.
"Na kwa wakati ule hasa ilikuwa ni benki za biashara ndizo zilikuwepo, baada ya kuanzishwa kwake na kanda maalum kuanzishwa hasa Kanda ya Afrika Mashariki (East Africa Community), chuo kilianza kutoa kozi kwa wafanyakazi wa benki kuu kutoka East Africa Community kwa lengo la kuwapa uzoefu na weledi katika masuala ya benki kuu.
"Na hizo kozi zilizokuwa zinafundishwa na chuo chetu, ni zile kozi ambazo zilikuwa zimekubaliwa na magavana wa nchi za Afrika Mashariki na, Endelea kutazama mahojiano hapa chini;