DAR-Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanatarajiwa kukutana Agosti 27 hadi 30, 2024 katika kikao kazi kitakachofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.