Kituo cha Biashara Ubungo (EACLC) kufunguliwa Oktoba

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji wa Tanzania, Prof.Kitila Mkumbo amewaita Watanzania kuchangamkia fursa katika Kituo cha Biashara Ubungo (EACLC), jijini Dar es Salaam ambacho ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 90.
Amesema, asilimia 95 ya maduka 2,060 yaliyopo kituoni hapo yametengwa kwa Watanzania hivyo hawana budi kuwekeza kwa ajili ya maendeleo yao pamoja na Taifa.

Waziri huyo ameyabainisha hayo alipopokea ujumbe wa wawekezaji kutoka Jiji la Weihai la China waliofika kituoni hapo kwa ajili ya kufungua eneo la biashara na kuwekeza.

"Faida yake katika uchumi ni kubwa kwani Watanzania zaidi ya 15,000 watapata ajira za moja kwa moja lakini pia kitalipa mwonekano mzuri jiji letu.”
Amesema ni sehemu muhimu kwa Watanzania kukuza uwezo wa kibiashara ndani, Afrika na duniani kwa ujumla.

Kuhusu kufunguliwa Meneja wa Kituo hicho, Victoria Mombury amesema kitafunguliwa Oktoba,2024 kwani hadi sasa kimeshakamilika kwa asilimia kubwa.

Akizungumzia ujumbe huo kutoka Weihai amesema wanajihusisha na bidhaa za viwanda na uzoefu wa teknolojia pia huduma za usafirishaji wa bidhaa kutoka China kuja Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news