MOROGORO-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Kiwanda cha sukari Mkulazi kitatoa ajira 11, 315 kwa watanzania ifikapo Disemba mwaka huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wakiwa katika hafla ya uzinduI wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, Mbigiri Mkoani Morogoro, tarehe 7 Agosti, 2024.
Aidha, amesema kukamilika kiwanda hicho kutaongeza wigo wa fursa za ajira hususan kwa vijana katika shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda na mashamba ya miwa.

Amesema kuwa, ujenzi wa mradi huo umegharimu shilingi bilioni 344, ambazo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda na kazi za kilimo, miundombinu ikiwemo ujenzi wa njia ya umeme.

