LNG ni kipaumbele cha Serikali,majadiliano na kampuni za Kimataifa yanaendelea-Mheshimiwa Kapinga

DODOMA-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali inaendelea na majadiliano na Kampuni za Nishati za Kimataifa (International Energy Companies - IEC’s) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia kuwa Kimiminika (LNG) na yakikamilika Serikali itaupeleka kwenye hatua inayofuata.
Mhe. Kapinga amesema hayo leo Agosti 29, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Joseph Khenani aliyetaka kufahamu lini Serikali itapeleka bungeni mkataba kati ya Tanzania na Wawekezaji wa Gesi asilia wenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 70 kwa ajili ya kujadiliwa.

"Mradi huu unamanufaa makubwa sana kwa Taifa letu, majadiliano haya ni muhimu kwa sababu ndio yanayoweka msingi wa kodi, mirabaha pamoja na ulinzi wa vigezo wa Nchi kunufaika kiuchumi,"amefaganua Mhe. Kapinga.

Amelihakikishia Bunge kuwa,suala la mradi wa LNG ni kipaumbele katika Serikali na majadiliano yanaendelea na yapo katika hatua nzuri.

Kuhusu kuagiza gesi ya LPG kwa mfumo wa uagizaji wa pamoja ili kuleta unafuu wa bei kwenye gesi, Mhe. Kapinga amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wanahakikisha soko la gesi linakuwa himilivu ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa kwa urahisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news