DODOMA,ZANZIBAR-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewakaribisha wananchi katika mabanda yao yaliyopo katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea viwanja vya Nzunguni jijini Dodoma na viwanja vya Dole, Kizimbani jijini Zanzibar ili kupata elimu na kufahamu huduma wanazotoa kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Wataalamu kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi katika viwanja vya Dole, Kizimbani, Zanzibar.
Wataalamu mbalimbali kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi katika viwanja vya NaneNane, Nzuguni, Dodoma.
Ikumbukwe kuwa, TMA ni mdau mkubwa katika sekta ya kilimo na mifugo nchini kwani, taarifa za hali ya hewa kilimo ni muhimu sana kwenye mipango na shughuli mbalimbali kwa mfano umwagiliaji ili kuhifadhi maji au nishati, kuchagua wakati unaofaa wa kutumia viuatilifu, matumizi ya mbolea, uzalishaji wa mifugo au uvuvi.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Maonesho ya Nanenane
Tanzania Meteorological Agency (TMA)